BAADA YA MISS TZ 2014 KUANDAMWA SANA MITANDAONI, MISS TZ 2012 AMEAMUA KUMSHAURI
Kama
na wewe unakerwa au haupendi jinsi ambavyo Miss Tanzania wa 2014 Sitti
Mtemvu amekua akiandamwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu umri
wake na elimu yake baada ya kushinda taji hilo weekend iliyopita basi
uko upande mmoja na Miss Tanzania wa 2013Brigitte Alfred.
Kupitia
page zake za twitter na Instagram Brigitte pamoja na mengine ameandika
>>> ‘Mazuri mengi yanawapita lakini inapotokea skendo mnajadili
milele ndio maana hatuendelei, natamani tungeweka hizi nguvu za matusi
kwenye vitu vya kujenga‘
Baada ya
hiyo sentensi Brigitte alimuandikia Sitti kwa kusema >>> ‘Sitti
usiwaruhusu watu wakuandame sana, ikizidi warudishie tu taji lao’
Kwenye
tweets nyingine za wiki hii baada ya Sitti kutangazwa mshindi Brigitte
aliandika ‘mngejua siasa za huko Miss World hata msinge jisumbua
kumshambulia huyu msichana kiasi hicho, mtihani wa Miss Tanzania sio tu
siku ya fainali ndio maana kunakua na camp ya siku 30′
No comments:
Post a Comment