ISABELA: WANAWAKE TUSHINIKIZE NDOA TUOLEWE
Na Mayasa MariwataMSANII Isabela Mpanda ambaye yupo kwenye mikakati mizito ya kuolewa na msanii mwenzie Luten Karama, amewataka wasanii wa kike kuwa makini pindi wanapoahidiwa kuolewa kwa kushikilia bango mpaka kieleweke kwa kuwa ndoa si lelemama.
Akibonga machache na paparazi wetu alisema, kinachowaponza wasanii wengi wa kike kuishia kuzaa bila kuolewa ni wengi kutotilia mkazo ahadi za ndoa wanazopewa na wenzi wao kwa kuamini mambo…
Na Mayasa Mariwata
MSANII Isabela Mpanda ambaye yupo kwenye mikakati mizito ya kuolewa na msanii mwenzie Luten Karama, amewataka wasanii wa kike kuwa makini pindi wanapoahidiwa kuolewa kwa kushikilia bango mpaka kieleweke kwa kuwa ndoa si lelemama.
Akibonga machache na paparazi wetu alisema, kinachowaponza wasanii wengi wa kike kuishia kuzaa bila kuolewa ni wengi kutotilia mkazo ahadi za ndoa wanazopewa na wenzi wao kwa kuamini mambo yataenda sawa pasipo kuwahimiza.
“Ndoa si lelemama! Maana wanaume kutoa ahadi ni jambo rahisi sana lakini kutekeleza shida, inabidi ufanye mengi ya kumvutia ili ashawishike ikiwemo upendo na nidhamu, vinginevyo tutaishia kutangaza ndoa hewa na kuzalishwa tu ndiyo maana nimeanza maandalizi mapema ya ndoa yangu na Karama,” alisema Isabela ambaye siku chache zilizopita alinaswa akisaka gauni la harusi.
No comments:
Post a Comment