MAKUBWA HAYA: PENZI LA WEMA NA DIAMOND KUOTA MBAWA, MAMA WEMA AFANYA SHEREHE!
Supastaa ‘grade one’ wa sinema za Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ akipozi.
CHEREKO chereko! Siku chache baada ya supastaa ‘grade one’ wa sinema za
Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ kummwaga King of Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond’, mama mzazi wa mwigizaji huyo, Mariam Sepetu ameangusha
sherehe ya nguvu kama ishara ya kuonesha ‘amekunwa’ na tukio hilo.
Kwa mujibu wa chanzo makini, kutokana na mama huyo kutobariki uchumba
wa mwanaye na Diamond ambaye pia anajulikana kwa jina la Dangote kwa
muda mrefu, habari za uchumba huo kuvunjika zilipochapishwa kwenye
Gazeti la Ijumaa ‘Kubwa’ toleo lililopita, moyo wake ulijawa na furaha.
“Mama Wema alichukizwa kwa kiasi kikubwa na mapenzi ya wawili hao
kutokana na kile alichoamini kuwa, Diamond hakuwa na mapenzi ya dhati
kwa mwanaye zaidi ya kutegemea nyota yake impe mafanikio ndiyo maana
akafanya pati hiyo fupi nyumbani kwake Sinza-Mori, Dar,” kilisema chanzo
hicho.
Wema Sepetu ‘madam’ akifurahi na mama yake, Mariam Sepetu
SHEREHE ILIVYOKUWA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga unga kwamba, sherehe hiyo ilikuwa ni ya
aina yake kwani mama Wema aliwaita mashosti zake, wakaandaa ‘menu’ ya
ukweli kabisa, wakasherehekea lakini bahati mbaya Wema hakuhudhuria.
“Wema hakuweza kuhudhuria sherehe hiyo kutokana na kubanwa na
majukumu mengine. Bi mkubwa aliwaita marafiki zake, wakafungua shampeni,
wakala, wakanywa na kucheza muziki kufurahia Dangote kupigwa chini,”
kilisema chanzo hicho.
Dangote wakati akiwa na Penniel Mungilwa ‘Penny’
MAMA NA CHUKI YA MUDA MREFU
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu motomoto kuwa, mama Wema alipiga
cherekochereko za kutosha siku hiyo kwani alikuwa akimchukia Diamond kwa
muda mrefu.
“Mama Wema chuki zake kwa Diamond hazitaisha kamwe kwa kuwa hampendi
tu kutokana na kuona mwanaye hasongi mbele kimaendeleo kama alivyo
Diamond ambaye akiachana na Wema mambo yake hayamwendei vizuri kama
anavyokuwa na mwanaye.”
Diamond wakati akiwa na Jokate Mwegelo.
MAMA WEMA ANENA
Baada ya wanahabari wetu kunasa maelezo hayo ya chanzo, walimvutia
waya mama Wema ambaye alikiri kufanya sherehe fupi baada ya mwanaye
kummwaga Diamond.
“Mimi naona huu ndiyo mwisho wa Wema na Diamond na siku zote nasema
hakuna uhusiano ukadumu bila baraka za wazazi, niseme tu, sitaki kumuona
ndugu yeyote wa Diamond kwangu, kama mahari wakatoe kwa Penny siyo kwa
mwanangu,” alisema mama Wema.
Wema Sepetu,'Madam' akiwa na Diamond Platinumz.
TUJIKUMBUSHE
Kumwagana kwa Wema na Diamond safari hii, ni mara ya nne. Awali
walimwagana, wakarudiana, wakamwagana tena, Diamond akatua kwa Jokate
Mwegelo, wakarudiana tena na Wema, wakaja mwagana tena, Diamond
akatambaa na Penniel Mungilwa ‘Penny’, wakamwagana, karudiana na Wema,
sasa wamemwagana tena.
No comments:
Post a Comment