Dondoo Kutoka Kikao cha Ndani ya Baraza la Mawaziri kilichofanyika jana Dodoma kilichofanyika
Ofisi za TAMISEMI.Kikao rasmi cha kujadili sakata la IPTL/ESCROW namna wahusika Watakavyowajibishwa au kuokolewa.
Misimamo ya Mawaziri tofauti tofauti.Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu waziri wa Fedha anatajwa kuwa Waziri wa kwanza kuonesha msimamo wake wazi wazi kuwa Sakata la IPTL/ESCROW ni hujuma dhidi ya Uchumi wa Nchi.acharuka,AAGIZA MALI ZOTE NA PESA ZOTE ZILIZOLIWA, ZILIZOTAWANYWA ZIKAMATWE.Naibu huyu ambaye mara kadhaa amekuwa akitajwa na vyombo vya habari kwa juhudi zake za kuokoa matumizi mabaya ya fedha na hata Watanzania wengine kuamua kumbatiza jina la Sokoine wa pili ikiwa ni kufuata nyayo za aliyewahi kuwa Kiongozi Makini Nchini hayati
Moringe Sokoine. Mwigulu ndani ya kikao hicho cha siri anatajwa kuendeleza ujasiri wake kuhusu mambo yenye masilahi ya Taifa. Wakati watu na tetesi mbalimbali zilikuwa zinaongelea kujiuzulu, Mwigulu
amejitokeza kwenyw kikao hicho na kusema CAG ameshamaliza utata, sasa mali zote, fedha zote
za IPTL zikamatwe na wahusika wote wakamatwe. Nanukuu kama nilivyosikia"Tumezoea kusema eti
tumewajibisha watu kwa wao kujiuzuru, "Kujiuzuru ni kupewa Likizo ya kwenda kula fedha ulizo
ziiba"anasema Mwigulu, Hili ni jambo la mazoea, sasa, CAG ameshasema pesa zile zilikuwa mali ya
umma, sasa zikamatwe zote, na wahusika wote wakamatwe" Mwigulu alienda mbali zaidi na kusema hata
ambao walishastaafu na wamehusika kulihujumu taifa wakamatwe na akaunt zao zikamatwe,
zifilisiwe zirudishwe kwa wananchi. Katika hatua nyingine Naibu huyo anayeshughulikia
mambo ya sera, Mwigulu ameagiza mtumishi wa TRA aliyepewa 1.6bilion afukuzwe kazi, akamatwe,
na akaunti ifilisiwe fedha irudi serikalini. Pia mitambo ya IPTL ikamatwe irudishwe serikalini.
Utamaduni wa watu kujiuzulu na kuhesebu kuwa ni adhabu ni jambo la zamani, sasa ili kukomesha
wizi, uzembe na ufisadi sasa tuwakamate wahusika wote, tuwafilisi na tuwaweke ndani na
tuwafunge.
No comments:
Post a Comment